Arsenal
Arsenal wanamtaka winga anayeuzwa kwa £15 na Valencia Juan Mata ili acheze na Samir Nasri. (Daily Mirror)
Southampton wameichekea nje ofa ya Arsenal £6m ili kumpata winga Alex Oxlade-Chamberlain. (Daily Star)
Barcelona watawatoa mabeki wake Maxwell au Eric Abidal ili kumpata kiurahisi Cesc Fabregas. (Metro)
Chelsea wanamkimbizia kipa wa Genk anayedaiwa kuuzwa kiasi cha pauni millioni 9 Thibaut Courtois kama mrithi wa Petr Cech. (The Sun)
West Ham wanaandaa kitita cha £7.5 million ili kuwasajili Joe Cole and Paul Konchesky . (Caught Offside)
Patrick Vieira yuko tayari kumshushua kocha wake wa zamani Arsene Wenger kwa kuchukua jukumu la kuwa kwenye bechi la ufundi wa Manchester City (Goal.com)
Aston Villa wanatumaini kumpata Shay Given kwa £4 million kutoka Man City. (The Sun)
United wako tayari kutoa ofa kati ya £10-12 million, pamoja na wachezaji wawili ili kumpata kiungo Luka Modric. (Caught Offside)
Kocha wa Leicester Sven-Goran Eriksson anampango wa kumsaini Owen Hargreaves. (The Sun)
Sunderland wamepooza kidogo katika kumsajili kiungo Darron Gibson. (Northern Echo)