Chelsea yampata Mata
Klabu ya soka ya Chelsea imefanikiwa kumpata yosso wa Hispania Juan Mata. Mata ambaye alikuwa akiwindwa na Arsenal sasa amesaini Chelsea na atajiunga na akina Oriel Romeu, Romelu Lukaku na Thibaut Courtois.
Messi: Man U tu ndio inayotisha
Mshambuliaji nyota wa Barcelona hivi juzi alikaririwa akisema kuwa Man Utd tu ndio inayowanyima usingizi na sio Real Madrid.
Daglish bado na wengine
Kocha aliyeleta mapinduzi Liverpool King Kenny, anaoneka bado hajatosheka na usajili alioufanya baada ya kuwasaini Charlie Adam, Jos'e Enrique, Doni na Jordan Henderson. Kocha huyo anavumishwa kuwataka Rodalega, Rowwdell na Kevin Doyle.