
Sasa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England Manchester United imeamuandalia kiungo wa kimataifa wa England na klabu ya Aston Villa Ashely Young(pichani).
Young ambaye amekua kwenye rada ya Manchester United kwa muda wa mwaka sasa anajulikana kwa kasi, krosi na mashuti maridadi. Young pia alifunga bao safi dhidi ya Uswisi na kurudisha matumaini ambayo hatahiyo iliambulia viporo kwa sare ya 2-2.

Kuachana na Young United pia inahusihwa na kumnasa kipa wa Atletico Madrid David Da Gea kwa paundi millioni 18, kiungo wa Everton Jack Rodwell kwa paundi millioni 20, Karim Benzema million 20, Kiungo wa Tottenham Hotspurs Luka Modric huku kukiwa na habari mbaya kuwa kiungo wa Sunderland Henderson asaini Liverpool kwa pauni millioni 20.