Saturday, June 18, 2011

Blue ndio rangi ya Modric'



Spurs wangependa kumshikilia kiungo wa Luka Modric' ila yeye mwenye angependa KUSEPA na kutimkia The Blues.

Modric,25 aliweka mambo wazi kwa kumwambia Mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy kuwa angependa kuhamia Chelsea. Alisema, "kama timu yoyote ingekuja kuniulizia kwa bei nzuri, nitaondoka! aliendelea kusema kuwa "Chelsea ni klabu nzuri yenye mwelekeo na matumaini ya kuchukua ubingwa.


MAONI YA MWANDISHI

Habari hizo ni mbaya kwa Spurs ambao wangependa kumbakisha mchezeshaji huyo. Kuna uwezekano mkubwa kuwa Modric', Gareth Bale na Rafael Van der Vart wangetimka kwani tokea mwanzo mwa msimu walitangaza kuwa kama Spurs ingeshindwa kutinga katika Klabu Bingwa Ulaya basi wangeondoka!