Saturday, June 18, 2011

Barca mambo shwari!

Barcelona wamesonga mbele zaidi ya Man Utd katika kinyanganyiro cha winga kutoka Chile, Alexis Sanchez.

Miamba hiyo ya Uhispania wako katika mpambano wa wakali watano ambao ni Man Utd, Juve, Inter Millan na Man City kugombania saini ya winga huyo anayechezea klabu ya soka huko Italia, Udinese.

Wakala wa winga huyo amependekeza na kuweka wazi kuwa Barcelona ndio walio na nafasi kubwa!