Saturday, February 26, 2011

Redknapp: £11m kwa Bojan.


Tottenham wameandaa kumnunua mshambuliaji wa Barcelona Bojan Krkic.

Mchezaji huyo mwenye miaka 20 ameona nafasi ya kikosi cha kwanza kuwa kidogo baada ya kucheza vizuri kwa Pedro na Ibrahim Affelay kutokea PSV Eindhoven.

Tottenham wameonyesha nia ya kumsaini straika wa Barca, Bojan. Huku kocha wa Tottenham Hotspurs, Harry Redknapp amekarishwa na jinsi timu yake imeshindwa kushambulia nyavu na anadhani kuwa Bojan ndio suluhisho baada ya kinda mwenye kusema, "ninaipenda sana Premier League.

Harry Redknapp anaweza kuwa anaamini kumpata fowadi huyo kwa kiasi cha £11m kwenda White Hatt Lane na anaweza kumpatia nafasi za kucheza kwenye kikosi cha kwaza. Na pia amesema atauza mmoja wa fowadi wake ambao ni Robbie Keane, Peter Crouch, Roman Pavluchenko au Jermain Defoe kama atapata mchezaji mzuri.