
Samir Nasri amekubali kusaini mkataba mpya na Arsenal ambao utawakatisha tamaa timu zozote zilizo dhani zitampata kiungo huyo katika majira ya joto (summer).
MFrance huyo ameripotiwa kusaini mkataba na Gunners ambao unazidi £26m -ambao ni zaidi ya £100,000 kwa wiki.
Inakuja na zawadi ya kuwa na msimu mzuri na Arsenal kwa kiungo huyo mwenye miaka 23, ambapo mkataba wake ulikuwa £60,000 kwa wiki. (The Sun)
Kwanza Theo Walcott hatacheza kwenye mchezo wa Wembley halafu nahodha Cesc Fabregas hatacheza baada ya kutolewa mapema katika mchezo dhidi ya Stoke City.
"Hebu piga mahesabu: Ramsey alivunjika mguu dhidi ya Stoke msimu uliopita. Halafu Walcott na Fabregas wameumia. Hivi ni kwanini Stoke tu!!!!!!!!!!!!! " ni mimi Boniface mwandishi wa blog hili