Roy Hodgson amesisitiza kwamba mashabaki wasijawe na hasira "Klabu nyingi zimeendeshwa chini ya uongozi mzuri lakini kocha akiingia kwenye kuwasajili wachezaji, anaweza akawasajili wachezaji lakini inatokea kwamba mchezaji uliyemnunua hakuwa anayetakiwa kuwapo pale kwaio nawaomba mashabiki kwamba watulie itachukuwa mda lakini Liverpool itakuwa
"Lakini tunachotakiwa kujua unaposajili wachezaji kuna wachezaji wadogo ambao wakikuzwa watacheza mpira vizuri zaidi. Kama hapa Liverpool sasa tunao wachezaji wadogo kama (Jonjo) Shelvey na (Martin) Kelly na ndio maana ukienda kusajili wachezaji unatakiwa kuwafikiria wachezaji wadogo kama hawa kwamba Je, atapata nafasi ya kucheza na kukuzwa na kuwa staa wa baadaye au unaangamiza kiwango chake kwa kuwaleta wachezaji wakubwa?.