Monday, December 6, 2010

FERGUSON AHAKIKISHA WELBECK NI UNITED



Kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson ameyaondoa mipango yote kocha wa Sunderland Steve Bruce ya kutaka kumchukua mchezaji wake Danny Welbeck. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 20 amabae yuko kwa mkopo katika klabu ya Sunderland na pia anacheza vizuri sana akiwa katika klabu hiyo.Kocha wa Sunderland Steve Bruce amesema waziwazi kwamba angependa kumnunua Danny Welbeck lakini amedhihirisha ya kwamba kuna uwezekana mdogo sana wa kumnunua mchezaji huyo ambaye makao yake makuu kabisa ni Manchester United.
Lakini Ferguson, ambaye amependezwa na kiwango cha mchezaji huyo amewaambia mashabiki wa Manchester United kwamba wasiogope kuhusu Danny Welbeck na kwamba amewahakikishia ya kwamba Welbeck atarudi United na kucheza kama kawaida.
Ferguson alisema ‘Welbeck ni mchezaji mzuri na pia ana kipaji cha kucheza lakini tatizo lilikuwa hapa United tuna wachezaji wazuri zaidi kwaio tunatakiwa tusubiri mpaka zile mechi ndogo kama za Carling cup, FA cup na nyinginezo ambazo zinatokea mara chache sana.

Ferguson aliendelea kusema ‘Welbeck alichezea timu ya vijana wadogo miaka miwili na nusu iliyopita na pia alikuwa na tatizo la kukuwa kimisuli kwaio tulikaa na kumwambia itabidi uende Preston naye alifurahia sana lakini alivyoenda Preston aliumia goti ikabidi afanyiwe Operation, lakini sasa tunaona jinsi anavyoendelea kukuomaa na kufanya vizuri. Kufunga magoli na hapa Premeir League kwa sasa ni tabu lakini Welbeck ana mbinu na hata kufunga goli zidi ya Chelsea na kumfunga Cech ni kitu ambacho hapa United tunamfurahia Welbeck.