KLABU ya soka ya Real Madrid inakula njama kumpata beki wa Man U Nemanja Vidic kwa kutokumruhusu Karim Benzema atue Man U. Safu ya ushambuliaji kwa Man U imekuwa tatizo kwani imekuwa sana mabegani mwa mshambuliaji wa Man U, Wayne Mark Rooney msimu uliopita.
Mshambuliaji wa Bulgaria na Manchester United Dimitar Berbatov ameshindwa kulinganisha kiwango na mshambuliaji mpya wa Mexico Javier Hernanes ambaye anafikiriwa kuwa atakuwa kinda wa ukweli kama moto uotao mbali.