
Mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney amekataa marumbano kuwa England ilicheza chini ya kiwango dhidi ya United States of America (U.S.A) kwenye mechi ya ufunguzi.

Gerrard aliipa Uingereza goli la kwanza baada ya kufunga ndani ya dakika tano ambacho kinaaminika kuwa goli la haraka kwenye Mashindo ya Kombe la Dunia Sauzi 2010 huko Rustenburg. Hatahivyo kipa wa Westham, Rob Green alifanya makosa na kumruhusu kinda wa Fulham Clint Demsey asawazishe mambo.