Sunday, October 11, 2009

MHHHH! ACHA NISEME UKWELI


Mshambuliaji wa klabu ya Everton LOUIS SAHA amethibitisha jinsi alivyokuwa amekata tamaa ya kuendelea kucheza soka na kukaribia kustaafu kucheza mchezo huo.Saha amesema alifikiria kuacha mchezo wa soka kutokana na masharti aliyopewa akiwa na klabu yake ya zamani ya Manchster utd baada ya kuambiwa afanye mazoezi bila ua kulipwa posho yake na alilazimika kuingia mkataba wa miaka miwili kuendelea kuichezea klabu hiyo ambao angelipwa kutokana na mechi atakazocheza.Mshambuliaji huyo wa kimataifa toka nchini Ufaransa ameumia mara 23 katika miaka minne aliyoichezea klabu ya Manchester United kabla ya kusajiliwa na klabu ya Everton mwaka 2008.