
Klabu ya JUVENTUS inafanya mipango ya kumsajili kiungo wa kimataifa toka Argentina anayeichezea klabu ya Liverpool Javier Mascherano.Klabu ya Juve iliwahi kutaka kumsajili kiungo huyo alipokuwa anaichezea klabu ya West Ham UTD kabla ya kusajiliwa na klabu ya Liverpol mwezi January mwaka 2007.Mascherano ambaye tayari ameanza kuvutiwa na klabu ya Barcelona anamiliki paspoti ya nchini Italia amekuwa akihusishwa na taarifa za kutaka kuondoka Anfield lakini mkataba wake ambao unafikia kikomo mwaka 2012 umekuwa kikwazo kwake.