Sunday, October 11, 2009

JE! EVRA NI MFALME NJOZI.


Beki wa kimataifa toka nchini Ufaransa anayeichezea klabu ya Manchester utd PATRICE EVRA ametabiri huenda wakakutana a na klabu ya Real Madrid iliyomsajili winga wao wa zamani Cristiano Ronaldo katika mchakato mzima wa michuano ya klabu bingwa barani ulaya msimu huu.Evra amekumbushia kuwa aliwahi kucheza nae akiwa katika kikosi cha timu ya taifa cha ufaransa chini ya umri wa miaka 21 na kutokana na kucheza nae Manchester hana wasiwasi wowote wa kumdhibiti iwapo watacheza na Madrid.Kwa upande mwingine amekiri wazi kwamba alisikitishwa kutokana na winga huyo kuhamia Real Madrid na kuongeza kuwa kuna wakati mtu anatakiwa kukubaliana na mazingira kadri yanavyoruhusu.