Friday, July 8, 2011

Vidal atawacosti sana!




Bayern Leverkusen imesema kuwa haitakubali kiasi kidogo kwa klabu yoyote itakayokuja kumuuilizia kiungo wao mahiri Alturo Vidal.


Mchezaji huyo ambaye ni raia wa Chile yupo pamoja na timu yake ya taifa kwenye mashindano ya Copa America amedaiwa kuhusishwa na mpango kwenda Arsenal, Juventus na Bayern Munich.


Ila klabu hiyo imesema haita muuza kwenda kwa mahasimu wao Bayern Munich na kusema itakubali ofa ya pauni millioni 19 kwa klabu nje ya Ujerumani.