US Palermo kutoka Italy ya Serie A wameripotiwa kumlenga mshambuliaji wa Man U Federico Macheda mwenye umri wa miaka 19 kwa ajili ya kumrithi Massimo Maccarone mwenye miaka 31.
Gazeti la Corriere dello Sport linataja ya kwamba Macheda amewaambia familia yake na wakala wake kwamba anataka kurudi nchini Italia.
Bosi wa Manchester United Sir. Alex Ferguson ameonekana kukubaliana na jambo hilo la Macheda kuondoka lakini ni kwa mkopo tu kama alivyofanyiwa Weldeck ambaye kwa sasa yuko Sunderland.
Macheda alionyesha kiwango chake katika mechi ya Aston Villa ambapo alifunga goli ambalo lilimfanya Ferguson kuchukua kombe katika msimu huo.Ameichezea Manchester United mara nisa msimu huu na kufunga bao moja na kutengeneza goli moja lakini bado amejikuta akiwa nyuma kwa washambuliaji kama Javier Hernandez , Dimitar Berbatov na Wayne Rooney. Macheda anawaniwa na timu kama Lazio Roma, Juventus na AC Milan.