Monday, December 6, 2010

VERMAELEN ASEMA KWELI JUU YA CESC


Thomas Vermaelen amesema ya kwamba Cesc Fabregas amewaambia wachezaji wenzake wa timu ya Arsenal kuwa alitaka kujiunga na Barcelona kabla ya msimu huu kuanza.
Kiungo huyo wa Spain Fabregas, ambaye ni nahodha wa Gunners, alihusishwa na mpango wa kujiunga na mabingwa hao wa La Liga Barcelona, ambacho kilimweka kocha wa Arsenal Arsene Wenger kusima na kuanza kumtetea nahodha wake asiondoke na pia hana hata mpango wa kujiunga na Barcelona. Fabregas, ambaye alijiunga na Arsenal akiwa moto unaootea mbali akitokea kituo cha kuwazalisha vijana wa dogo wa Barca, alikubali kujiunga lakini kiupana alitegemea kuondoka Camp Nou msimu uliofuata.

"Lakini Cesc bado ana hamu ya kujiunga Barcelona na bado ipo kwenye moyo wake na DNA yake, itakuwa vigumu sana kumfanya asahau kuhusu Barca” alisema Vermaerlen Aliendelea kusema “Alipenda kujiunga na Barca msimu uliopita alituambia ukweli katika vyumba vya kubadilishia lakini hiyo ni kama historia, lakini sasa yuko 100% tayari kukaa na Arsenal na kuifanya ichukue ubingwa kama nahodha.