Thursday, December 16, 2010

Bale:Siondoki hata kwa dawa


Mchezo safi aliocheza Bale dhidi ya Inter Milan umewashtua wapenda mpira huku Real Madrid na Barcelona wakiwa tayari kutoa paundi millioni 50 kama ilivyo ripoti kwenye www.thesun.com.

Lakini Bale mwenye miaka 21 alisema: "Ninafuraha Tottenham na sioni sababu ya kwenda sehemu nyingine. Kuna wachezaji wengi ambao wamesaini mikataba mirefu ndani ya klabu na hicho kinasababisha klabu iwe na amani.

"Tottenham walionyesha dhidi ya Inter kwamba inaweza kushindana dhidi ya timu yoyote kubwa duniani na kwanini niondoke?