Rafael van der Vaart amevumbua wazi kwanini aliikataa Liverpool kukubali kujiunga na Tottenham.
Mholanzi huyo ambaye alijiunga na Tottenham katika dakika za mwisho kabisa kabla la dirisha la usajili kufungwa baada ya Harry Redknapp kumnyakua ili kupata hiduma yake katika nafasi ya kiungo.Inasemekana kwamba kiungo mchezeshaji huyo alikuwa abakie Real Madrid kwa kuwa hakukuwa na makubaliano yoyote kumtoa Rafael Van der Vaart kutoka Bernabeu.
Hata hivyo, Spurs walimpata katika njia ya ajabu kwasababu hakuna mtu aliyetegemea Van der Vaart kumaliza makubaliano katika hatua za mwisho za kufungwa kwa dirisha la usajili..Redknapp alisisitiza kwamba Bayern Munich ndio klabu ambayo walikuwa wakiwa na percent kubwa ya kumpata kiungo mchezeshaji huyo lakini katika dakika za mwisho Spurs ndio walioshinda mechi hiyo.
Lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 amesema siyo tu Bayern Munich iliyokuwa ikimhitaji ila Liverpool pia ilikuwa ikihitaji huduma zake. Van der Vaart alisema: "Liverpool walinihitaji,Bayern hawakunihitaji sana.”Lakini siku ya mwisho lazima uchague kitu roho inataka, mimi nilifurahia jinsi Totten walivyokuwa wanacheza na pia chini ya kocha wao Redknapp ndio maana nilijiunga Spurs.