Birmingham wanaweza kumsaini mshambuliaji wa Tottenham Roman Pavlyuchenko.(News of the World)
Tottenham wanamtaka kipa wa Udinese Samir Handanovic(The People)
Benni MacCarthy anaweza kwenda Portsmouth kutoka Blackburn January(The People)
Wolves wanaweza kumsaini beki Craig Gadner kwa paundi millioni 2 (The People) 

Kocha wa Everton David Moyes anamwania “staa” wa Benifica Javi Garcia na Cris Eagles kwa millioni 2 na O’Neil(News of The World) na (The People)

Kocha Roberto Martinez wa Wigan anamfuatilia mshambuliaji wa Espanyol Raul Tamudo(The People)

Kocha wa Sunderland Steve Bruce ana ndoto za kumnasa kiungo Maynor Figuera kwa millioni 6 na kiungo wa Cardiff Peter Whittingham. (The People)

Beckham anatarajia kujiunga AC Millan na kustaafu soka la Kimataifa baada ya World Cup(Daily Mirror)

Beki Rio Ferdinand ameumia sehemu za mgongo na kuwa nje kwa miezi miwili(News of The World)

Man Utd wamekanusha habari za kutaka kumuuza winga wao Louis Nani bali kasha saini miaka minne(The People)

Kocha Phil Brown atapewa muda kukaa ndani ya klabu, na kama hamna mabadiliko atafukuzwa(News of The World) na (The People)

Winga Luca Modric atakuwa nje kwa mwezi baada ya kuvunjika mguu. (News of The World)

Real Madrid itabidi kuchukua Jose Mouhrinho kama kocha Manuel Pellegrini hataleta mabadiliko. (News of The World)

Kocha mpya wa Middlesbrough amepewa millioni 15 ili ya kununua na kuuza wachezaji. (News of The World)