Saturday, November 7, 2009

KOMBE LA LIGI YA UINGEREZA NDANI YA BONGO.




Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya Barclays nchini Bw. Rashed Bade kulia na mwenyekiti wa Baraza la Michezo nchini BMT Kanali Idd Kipingu wakifunua kitambaa ili kuonesha kombe la Ligi kuu ya Uingereza (English Barcklays Premier Ligue Cup) mbele ya waandishi wa habari kwenye Hoteli ya New Africa jijini leo, kombe hilo litakimbizwa maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam kwa siku mbili mfurulizo ili kuwapa fursa mashabiki mbalimbali wa timu za Uingereza waliopo nchini kuliona.



Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa(BMT)Kanali Mstaafu.Iddi Kipingu(kushoto) na Mmoja wa Walinzi wa Kombe la Ligi Kuu ya Uingereza, Keith Russel wakiwa wameshikilia kombe hilo baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Julius Nyerere,mapema leo asubuhi kwa ziara maalum ya kuhamasisha michezo nchini.