Saturday, March 31, 2012

Mmmh??



Tuesday, August 30, 2011

Anzhi wapania kumsaini Vidic




Klabu ya Urusi Anzhi Makhachkala imeanzisha mpango wa kushtukiza wa kumsaini beki mahiri wa kati wa Man Utd Nemanja Vidic'.


Anzhi ambayo imeshamnunua straika hatari wa Kameruni Samuel Eto'o kwa pauni millioni 20, timu hiyo inataka timu hiyo iwe hatari.


Manchester United ilimsajili beki huyo kutoka Sparktar Moscow kwa pauni millioni 7

Mertesacker afanyiwa vipimo London



Beki mahiri wa klabu ya Wender Bremen Per Mertesacker ameruhusiwa na timu yake ya taifa kwenda London ili kufanyiwa vipimo ili kumaliza uhamisho wake kwenda Arsenal.


Kocha wa Ujerumani, Joachim Low alisema kuwa: "Alinipigia jana usiku kuniambia".Raia huyo wa Ujerumani alisema ana furaha Bremen ila hakutaka kukataa kuondoka.


Uhamisho huo utamkosti Wenger euro 10(pauni million 8.8)

Monday, August 29, 2011

Man U yaua kinoma-noma













Manchester United 8-2 Arsenal

Old Trafford

Friday, August 26, 2011

FERGIE aja juu kwa FA



Kocha wa Manchester United Sir. Alex Ferguson amewajia kuu Shirikisho la Soka Uingreza (FA) na kuwaambia wanaitibu timu yake kama s**t.


Man U msimu uliopita walikuwa na malumbano mengi na FA na sasa hataki itokee tena.


Man U imewatoa wachezaji nane kwenda England kama Danny Welbeck, Tom Clevery, Phil Jones, Rio Ferdinand, Wayne Rooney, Ashley Young, Cris Smalling na Michael Carrick.



Nasri ndo wamwisho!!!!!




Kocha wa Man City Roberto Mancini amesistiza kuwa kiungo Samir Nasri ndiye mchezaji wa mwisho kumsajili.




Man City inayojuliakana kama timu inayopenda hela, imewasajili wachezaji wengi wakubwa na wameweza kunyakua taji lao la kwanza kwa miaka 35.




BREAKING NYUZ:


Kiungo Samir Nasri amesema kuwa, "Man Utd wasubirie vipigo tu"

Bolton wakataa ofa ya Arsenal



Kocha wa Bolton Wanderers Owen Coyle amethibitisha kuwa wamekataa ofa ya Arsenal kumyakua beki wao mahiri Gary Cahill.


Mwingereza huyo ambaye anahusishwa na mpangi kwenda Arsenal, Man City na Liverpoo na hata Manchester United. Amekuwa kati ya mabeki hodari Uingereza tangu alivyojiunga na Aston Villa.


Hata hivyo Arsenal wanahusishwa kupeleka 7M.

Nasri: City tu



Kiungo mpya wa Manchester City, Samir Nasri amesema kuwa alikuwa na wazo moja tu nalo tu ni City na sio mahasimu wao United.


Alisema kuwa hata kama kocha wa United, Sir. Alex Ferguson angetoa ofa kubwa angekwenda Man City


Alisema kuwa "Nimefurahi kujiunga na Man City kwani kuna wachezaji wazuri tu"








Spurs yampata Adebayor.

Mshambuliaji wa soka wa Manchester City, Emmanuel Adebayor kwa mwaka mzima kwa mkopo.

Mshambuliaji huyo wa Togo, amekuwa akisugua benchi alivyokua Man City mpaka alivyotolewa kwa mkopo kwenda Real Madrid.


Redknapp alisema "kama mashabiki wa Arsenal hawampendi basi wa kwetu watampenda.




Aquilani asepa.



Kiungo wa AC Milan Alberto Aquilani ameondoka kwenda AC Milan kwa mkopo wa mwaka mzima.


Kiungo huyo amekuwa hapangwi kwa mda mrefu amekuwa akivumishwa kwenda Fiorentina kwa muda mrefu ila Liverpool imekataa kumuuza kabisa-kabisa.

Makundi ya Champions League.




Group A


Bayern Munich

Villareal

Man City

Napoli


Group B


Inter Milan

CSKA Moskow

Lille

Trabzonspor


Group C


Man Utd
FC Basel

Benifa

Otelul Galati


Group D


Real Madrid

Lyon

Ajax

Dynamo Zagreb


Group E


Chelsea

Valencia

Leverkusen

Genk


Group F


Arsenal

Olympiakos

Marseille

Dortmund


Group G


Porto

Sharktar

Zenit St. Petersburg

APOEL


Group H


Barcelona

AC Millan

BATE Borisov

Viktoria Plzen

Thursday, August 25, 2011

Vijana wangu safi kabisa



Kocha wa Man Utd Sir.Alex Ferguson amesifia kikosi chake kilichopeta dhidi ya Tottenham Hotspurs kwa mabao 3-0.


Man Utd ambayo iliongozwa na kinda kama vile Tom Cleverly, Welbeck na De Gea walionyesha kandanda safi mbele ya mashabiki wao. Kocha wa Manchester United ana kibarua kigumu dhidi ya Arsenal na Chelsea ambazo zote zitakaribishwa Old Trafford.

Arsenal waponea chupuchupu!!!!













Udinese(Italy) 1-2 Arsenal(England)
Agg: 1-3







YANAYOJIRI ULAYA.





Chelsea yampata Mata
Klabu ya soka ya Chelsea imefanikiwa kumpata yosso wa Hispania Juan Mata. Mata ambaye alikuwa akiwindwa na Arsenal sasa amesaini Chelsea na atajiunga na akina Oriel Romeu, Romelu Lukaku na Thibaut Courtois.







Messi: Man U tu ndio inayotisha
Mshambuliaji nyota wa Barcelona hivi juzi alikaririwa akisema kuwa Man Utd tu ndio inayowanyima usingizi na sio Real Madrid.







Daglish bado na wengine

Kocha aliyeleta mapinduzi Liverpool King Kenny, anaoneka bado hajatosheka na usajili alioufanya baada ya kuwasaini Charlie Adam, Jos'e Enrique, Doni na Jordan Henderson. Kocha huyo anavumishwa kuwataka Rodalega, Rowwdell na Kevin Doyle.


Friday, July 8, 2011

Mambo yanayohusu usajili

Arsenal


Arsenal wanamtaka winga anayeuzwa kwa £15 na Valencia Juan Mata ili acheze na Samir Nasri. (Daily Mirror)


Southampton wameichekea nje ofa ya Arsenal £6m ili kumpata winga Alex Oxlade-Chamberlain. (
Daily Star)


Barcelona watawatoa mabeki wake Maxwell au Eric Abidal ili kumpata kiurahisi Cesc Fabregas. (
Metro)





Chelsea wanamkimbizia kipa wa Genk anayedaiwa kuuzwa kiasi cha pauni millioni 9 Thibaut Courtois kama mrithi wa Petr Cech. (The Sun)




West Ham wanaandaa kitita cha £7.5 million ili kuwasajili Joe Cole and Paul Konchesky . (
Caught Offside)




Patrick Vieira yuko tayari kumshushua kocha wake wa zamani Arsene Wenger kwa kuchukua jukumu la kuwa kwenye bechi la ufundi wa Manchester City (
Goal.com)


Aston Villa wanatumaini kumpata Shay Given kwa £4 million kutoka Man City. (
The Sun)


----------------------------------------------------------------
Manchester United


United wako tayari kutoa ofa kati ya £10-12 million, pamoja na wachezaji wawili ili kumpata kiungo Luka Modric. (
Caught Offside)


Kocha wa Leicester Sven-Goran Eriksson anampango wa kumsaini Owen Hargreaves. (
The Sun)


Sunderland wamepooza kidogo katika kumsajili kiungo Darron Gibson. (
Northern Echo)

Hulk: Njooni mnipate



Straika wa Porto Hulk amekaribisha timu yoyote ambayo inamtaka ikiwamo Chelsea. Raia huyo wa Brazil amedaiwa kuuzwa kwa pauni millioni 100 na kuweka rekodi.






Mchezaji huyo ambaye alisaini mkataba wa miaka mitano amekuwa na uhusiano mzuri na kocha wake Andre Villas-Boas. Mchezaji huyo alisaini mkataba huo May tu na Chelsea wana mpango wa kuuvunja mkataba huo.

Vidal atawacosti sana!




Bayern Leverkusen imesema kuwa haitakubali kiasi kidogo kwa klabu yoyote itakayokuja kumuuilizia kiungo wao mahiri Alturo Vidal.


Mchezaji huyo ambaye ni raia wa Chile yupo pamoja na timu yake ya taifa kwenye mashindano ya Copa America amedaiwa kuhusishwa na mpango kwenda Arsenal, Juventus na Bayern Munich.


Ila klabu hiyo imesema haita muuza kwenda kwa mahasimu wao Bayern Munich na kusema itakubali ofa ya pauni millioni 19 kwa klabu nje ya Ujerumani.

Saturday, June 18, 2011

RATIBA YA LIGI YATOKA!

Arsenal mechi 5 za mwanzo:

New C- A
Liverpool- H
Man U- A
Swansea- H
Blackburn- A

Chelsea mechi 5 za mwanzo:

Stoke-A
WBA-W
Morwich-H
Sunderland-A
Man Utd-H

LIVERPOOL mechi 5 za mwanzo:

Sunderland-H
Arsenal-A
Bolton-H
Stoke -A
Tottenham-A

Man Utd mechi 5 za mwanzo:

WBA- A
Tottenham-H
Arsenal-H
Bolton-A
Chelsea-H



Mambo yanaoneka mazuri kwa ofa ya Chelsea



Mambo yanaonekana mazuri kwa Chelsea baada ya Anderletch kuoneka kushawishika na Chelsea.


Kwa mara ya kwanza klabu ya Anderletch ya kukooo' Ubelgiji imetangaza kuwa katika mazungumzo na Chelsea kuhusu straika lao machachari Romero Lukaku. Lukaku, 18 anayesemekana kama Drogba mpya pia anawaniwa na klabu ya Man Utd na AC Milan.


MAONI YA MWANDISHI


Mbali na Lukaku Chelsea pia inamwania kiungo wa klabu ya Gent hukohuko Ubelgiji, de Bruyne mwenye umri wa miaka 19.

Barca mambo shwari!

Barcelona wamesonga mbele zaidi ya Man Utd katika kinyanganyiro cha winga kutoka Chile, Alexis Sanchez.

Miamba hiyo ya Uhispania wako katika mpambano wa wakali watano ambao ni Man Utd, Juve, Inter Millan na Man City kugombania saini ya winga huyo anayechezea klabu ya soka huko Italia, Udinese.

Wakala wa winga huyo amependekeza na kuweka wazi kuwa Barcelona ndio walio na nafasi kubwa!

Blue ndio rangi ya Modric'



Spurs wangependa kumshikilia kiungo wa Luka Modric' ila yeye mwenye angependa KUSEPA na kutimkia The Blues.

Modric,25 aliweka mambo wazi kwa kumwambia Mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy kuwa angependa kuhamia Chelsea. Alisema, "kama timu yoyote ingekuja kuniulizia kwa bei nzuri, nitaondoka! aliendelea kusema kuwa "Chelsea ni klabu nzuri yenye mwelekeo na matumaini ya kuchukua ubingwa.


MAONI YA MWANDISHI

Habari hizo ni mbaya kwa Spurs ambao wangependa kumbakisha mchezeshaji huyo. Kuna uwezekano mkubwa kuwa Modric', Gareth Bale na Rafael Van der Vart wangetimka kwani tokea mwanzo mwa msimu walitangaza kuwa kama Spurs ingeshindwa kutinga katika Klabu Bingwa Ulaya basi wangeondoka!

Thursday, June 9, 2011

Madrid yafanya mambo kimya kimya!




Klabu ya Real Madrid imedaiwa kumwalika nyota wa Santos ili kuzungumza jinsi ya kumpata.




RAC1 limebainisha kuwa makamu wa Rais wa Madrid Jose Sanchez amemwalika wakala wa mshambuliaji huyo Wagner Ribeiro ili kumwaga wino Santiago Bernabeu. Kuna habari hata mahasimu wao Barca wanamtaka kinda huyo wa Brazil Neymar!



Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich naye anahaha kumsaini ingawa Sanchez anaamiani Madrid ina nafasi kubwa.

United sasa waamua kufanya kweli.


Sasa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England Manchester United imeamuandalia kiungo wa kimataifa wa England na klabu ya Aston Villa Ashely Young(pichani).

Young ambaye amekua kwenye rada ya Manchester United kwa muda wa mwaka sasa anajulikana kwa kasi, krosi na mashuti maridadi. Young pia alifunga bao safi dhidi ya Uswisi na kurudisha matumaini ambayo hatahiyo iliambulia viporo kwa sare ya 2-2.


Kuachana na Young United pia inahusihwa na kumnasa kipa wa Atletico Madrid David Da Gea kwa paundi millioni 18, kiungo wa Everton Jack Rodwell kwa paundi millioni 20, Karim Benzema million 20, Kiungo wa Tottenham Hotspurs Luka Modric huku kukiwa na habari mbaya kuwa kiungo wa Sunderland Henderson asaini Liverpool kwa pauni millioni 20.



Wednesday, June 8, 2011

Real Madrid kuichokoza Manchester United.



Miamba ya Uhispania imedaiwa kumchukua nyota mwengine kutoka Manchester United Javier Hernandez.

Chicharito ni mmoja kati ya wachezaji wanaolipwa kiasi kidogo katika timu hiyo ambapo analipwa mshahara wa Sh. billioni 51.4

Kwahiyo miamba hiyo imedaiwa kuanda kiasi cha Sh.128.6 ili kumshawishi straika huyo ambaye ni tishio dunia nzima na kustaajabisha dunia nzima kwa kasi zake na umaridadi ambao umeisaidia inyakue kombe la 19 ambayo ni rekodi.

Sunday, May 8, 2011

Monday, April 11, 2011

TransfersOther gossipAnd finally



TRANSFER GOSSIP kutoka www.bbc.com

Manchester City boss Roberto Mancini ameingia katika mpambano wa kumsaini beki wa Bolton Gary Cahhil kwa £20m.
Full story: Daily Mirror

Inter Milan boss Leonardo anajipa moyo kuwa anaweza kumpata winga wa Arsenal kwenda San Siro kwa £31m.
Full story: caughtoffside.com

Manchester United wanapanga kumpata kiungo wa Real Madrid mwenye umri wa miaka 16 Enzo Zidane, mtoto wa shujaa Zinedine.
Full story: caughtoffside.com

Habari zote kutoka www.bbc.com

Redknapp: Nilimtaka Ferdinand



Tottenham boss Harry Redknapp amedhihisha kuwa alijaribu kumsaini defender wa Manchester United Rio Ferdinand mwanzoni mwa msimu huu.

Redknapp anampenda sana Ferdinand ambapo alimpa staa huyo wa England mechi yake ya kwanza ambapo alikuwa West Ham. Chifu wa Spurs anataka kuleta mastaa hapo Spurs hali akimlenga Ferdinand.

Hatahivyo, Redknapp alisema Manchester United walikataa kumuuza staa wao.

Kuszczak kuondoka?


Goalkeeper wa Manchester United Tomasz Kuszczak amethibitisha kuwa ataondoka Man U mwishoni mwa msimu.

Mpoland huyo hajaweza kumtoa Edwin van der Sar kutoka kwenye kikosi cha kwanza cha Old Trafford na ameamua kuindoka Old Trafford. Hatakama Mduchi mwenza Edwin Van der Sar kustaafu mwishoni mwa msimu, Kuszczack hatazidi kubaki kupigania kuwa kipa No.1

Sir Alex Ferguson anatarajia kuingia sokoni tena ili kumpata mbadala wa kipa huyo wa zamani wa Hertha Berlin na West Brom.

Cheki msimamo wa England

1 Manchester United 32 69
2 Arsenal 31 62
3 Chelsea 31 58
4 Manchester City 31 56
5 Tottenham Hotspur 31 53
6 Liverpool 31 45
7 Everton 32 44
8 Bolton Wanderers 32 43
9 Newcastle United 32 39
10 West Bromwich Albion 32 39
11 Fulham 32 38
12 Stoke City 32 38
13 Sunderland 32 38
14 Aston Villa 32 37
15 Blackburn Rovers 32 35
16 Birmingham City 31 35
17 Blackpool 32 33
18 West Ham United 32 32
19 Wolverhampton Wanderers 32 32
20 Wigan Athletic 32 31

Guardiola anaweza kuondoka


Kocha Barcelona Pep Guardiola amekataa kukana ya kwamba anaweza kuihama Nou Camp mwishoni mwa msimu ujao.

Habari hizozimewashtusha klabu kubwa Kama Chelsea, Manchester United and Arsenal.Kocha huyo mwenye miaka 40 alipatikana akisema kwenye moja ya vyomba vya habari Italy kuwa ataondoka Catalonia mwishoni mwa mwaka 2011/12.

Habari hizo huenda ni za ukweli kwani Pep Guardiola mwenyewe amesema kuwa kuna presha kubwa sana hapa Barcelona.

Man U kumtia Berbatov sokoni


Manchester United wanaripotiwa kuwaza kumuuza mfungaji wao Dimitar Berbatov kwenda Bayern Munich.

Mbulgaria huyo amejikuta akiwa bench mara kwa mara siku hizi. Hajaoneka akiwa na furaha kuhusu kukaa bench hususani ambapo amekuwa akifunga magoli mengi, ripoti zinadai kuwa Alianz Arena wako tayari kuofa €25m (£22m) ilikumpata straika huyo aliyekuwa Tottenham kabla ya kwenda Manchester kwa ada ya pauni millioni 30.5.

Monday, April 4, 2011

Hapatatosha Stamford Bridge!


Mbele yetu kuna pambano la kukata na shoka la CHELSEA NA MAN U, na kila siku mpambano kama huu ukitokea lazima mtu alie, je unafikiria nani atashinda!

Haya ni marudio ya fainali iliyochezwa Moscow ambapo Man U ilishinda kwa penati, nadhani Chelsea hawatataka haya yatokee tena. Je, Rooney atang'aa au Luiz atamuaibisha? Je, Drogba anamzidi Vidic maarifa? Je ni Torres au Chicharito ambao watafanya maajabu? Je Berbatov anaweza kujionyesha kuwa yeye ndio mfungaji bora Ligi kuu England?

Aaah! nimesema mengi sana sasa tuone nini hawa watu wanaweza kutufurahisha. Kombe la Mabingwa Ulaya ni Kombe la Maajabu sana.

Hii sio mechi ambayo itachezwa tu;

Tuesday April 5
5 Apr, 19:45 Real Madrid v Tottenham Hotspur Bernabéu, Madrid
5 Apr, 19:45 Internazionale v Schalke 04 Stadio Giuseppe Meazza, Milan
Wednesday April 6
6 Apr, 19:45 Chelsea v Manchester United Stamford Bridge, London
6 Apr, 19:45 FC Barcelona v Shakhtar Donetsk Camp Nou, Barcelona
Tuesday April 12
12 Apr, 19:45 Manchester United v Chelsea Old Trafford, Manchester
12 Apr, 19:45 Shakhtar Donetsk v FC Barcelona Donbass Arena, Donetsk
Wednesday April 13
13 Apr, 19:45 Tottenham Hotspur v Real Madrid White Hart Lane, London
13 Apr, 19:45 Schalke 04 v Internazionale Veltins-Arena, Gelsenkirchen

Manchester City yafanya mauaji.






Sunday, March 6, 2011

Shalke waongea juu ya Man U.


Schalke wamesema kwamba Manchester United wako makini kwa Neuer na wataangalia maelezo kama kuna hela au chochote kwa kipa huyo.


United wanatarajiwa kuwa sokoni kumsaka kipa mpya kwenye majira ya joto ambapo kipa wao atastaafu.


Mjerumani huyo amepangwa kuwa mmoja wa makipa waliotakiwa Old Trafford baada ya kuwa MKALI misimu iliopita.


Yuko chini ya mkataba na Schalke mpaka 2012 na klabu hiyo ya Bundesliga inataka kumkalisha hapohapo kipa wake.

Man C yapeta, Arsenal yapata aibu.




Manchester City 1-0 Wigan Athletic
City of Manchester (Eastlands)











Arsenal 0-0 Sunderland
Emirates Stadium