Kocha wa Man Utd Sir.Alex Ferguson amesifia kikosi chake kilichopeta dhidi ya Tottenham Hotspurs kwa mabao 3-0.
Man Utd ambayo iliongozwa na kinda kama vile Tom Cleverly, Welbeck na De Gea walionyesha kandanda safi mbele ya mashabiki wao. Kocha wa Manchester United ana kibarua kigumu dhidi ya Arsenal na Chelsea ambazo zote zitakaribishwa Old Trafford.