Sunday, June 6, 2010

Arsenal kukaza buti kwa Schwarzer



Arsene Wenger amepania kuziba tundu la kipa, kwani Arsenal ina tatizo kwenye safu ya ukipa. Wenger anamwazia kipa wa Fulham, Mark Schwarzer 37, na kupania kweli kweli kumpata.


Wenger ameamua kutoa millioni 4 kumnasa muAustralia huyo. Schwazer amekuwa na msimu mzuri Fulham kwa kuweza kuifikisha timu yake kwenye Fainali za EUROPA 2010.


Wakati huo huo Arsenal inaweza ikapata saini ya winga Joe Cole ambaye mkataba wake umekwisha na Chelsea inaonekana kuwa na mazungumzo naye. Joe Cole pia anawaniwa na Manchester United na Tottenham Hotspurs.