Thursday, December 24, 2009

EVERTON WAWATAKA WAWILI L.A GALAXY

Klabu ya Everton imethibitisha kuwa mbioni kumsajili kwa mkopo wa muda mfupi mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Marekani na klabu ya Los Angeles Galaxy Landon Donovan.



Hatua hiyo ya klabu ya Everton inamfanya mshambuliaji huyo kufuata nyayo za mchezaji mwenzake wa klabu ya Galaxy David Beckham ambae amesajiliwa kwa mara nyingine kwa mkopo na klabu ya AC Milan ya nchini Italia.

Mtendaji mkuu wa klabu ya Galax Robert Elstone amethibitisha kuwepo kwa taratibu za mshambuliaji huyo kutakiwa na meneja wa klabu ya Everton David Moyes.